Jangili Lanaswa na Meno ya tembo Vipande 21 huko Singida…!!
Jeshi la polisi mkoani SINGIDA limekamata vipande 21 vya meno ya Tembo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 43.
Nyara hizo za serikali zimekamatwa katika kijiji cha Mwamagembe wilayani Manyoni zikisafirishwa kwenda Itigi, mkoani Singida.
Mtu mmoja George James amekamatwa kwa tuhuma za kukutwa na meno
hayo ya tembo yakiwa yamehifadhiwa katika mabegi mawili ya kusafiria.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa katika kizuizi cha idara ya maliasili
kilichoko katika kijiji Ukimbu, kata ya Mgandu, wilayani Manyoni akiwa
katika gari aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T797CQL.
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida RPC Geofrey Kamwela (katika
video) amesema vipande hivyo 21 vina thmani ya zaidi ya shilingi milioni
43 na vyote vimehifadhiwa katika kituo cha polisi wilayani Itigi.”Meno
haya yanaashiria kuuwawa kwa tembo wanne”, alisema Kamanda James.
Vitendo vya ujangili wilayani MANYONI vimekuwa vikiongezeka ambapo
mwaka 2013 askari mmoja wa jeshi polisi alipoteza maisha katika
mapambano na majangili wilayani humo.
Tukio hili la limekuja wakati leo Rais Jakaya Mrisho Kikwete
amehudhuria mkutano maalumu wa kupambana na ujangili na biashara ya meno
ya tembo na pembe za Faru jijini London, Uingereza. Katika mkutano huo
amependekeza kupigwa marufuku biashara hiyo ili kuweza kudhibiti
ujangili duniani kote.
<iframe allowfullscreen="" frameborder="0" height="270" src="//www.youtube.com/embed
0 comments: